Jumapili 7 Juni 2026 - 20:00
Kuisaidia Iran dhidi ya uvamizi ni wajibu wa kisheria

Hawza/ Sheikh Salama Abdulqawi, mwanazuoni wa Ahlu Sunna kutoka Misri na mmoja wa maafisa wa zamani wa Wizara ya Wakfu ya Misri, akisisitiza kwamba; Iran ni nchi ya Kiislamu, ameeleza kuwa kuiunga mkono nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya Marekani na Israel ni “wajibu wa kisheria na Kiislamu”, na amesema kuwa Waislamu wanapaswa kusimama upande wa anayevamiwa, si upande wa mvamizi.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Islamic Analysis, wakati mvutano wa kisiasa na kijiografia katika eneo hilo ukiendelea, mwanazuoni mashuhuri wa Ahlu Sunna wa Misri ametoa matamshi muhimu kuhusu mivutano inayoendelea kati ya nchi za Kiarabu za Ghuba na Iran, ambapo ameeleza kuiunga mkono Iran kuwa ni “dharura ya kisheria na Kiislamu”.

Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha “Islamic Analysis”, Sheikh Salama Abdulqawi, mwanazuoni wa Ahlu Sunna wa Misri ambaye wakati wa urais wa Muhammad Morsi (2012–2013) alikuwa akihudumu kama msemaji rasmi na mshauri wa Wizara ya Wakfu ya Misri, katika mazungumzo yaliyotolewa kupitia kituo chake binafsi cha YouTube, alisisitiza kwamba; kuiunga mkono Iran dhidi ya mashinikizo na mashambulizi ya Marekani na Israel si upendeleo wa kisiasa, bali ni jukumu la kidini na kisharia.

Vita si kati ya nchi za Ghuba na Iran

Abdulqawi akijibu swali lililosema: “Kwa nini umechukua upande wa Iran dhidi ya ndugu zako wa nchi za Ghuba?” alisema kuwa; swali hilo lenyewe si sahihi, kwa sababu mzozo wa sasa si kati ya Iran na nchi za Ghuba.

Alisema: “Tupende tusipende, tuwe tunaipenda Iran au tusiipeende, mwisho wa yote Iran ni nchi ya Kiislamu, nchi hii imelengwa na mashambulizi ya nchi zisizo za Kiislamu kama Marekani pamoja na Netanyahu na washirika wake. Tukiangalia suala hili kwa mtazamo wa Sheria na itikadi ya Kiislamu, Muislamu kamwe hasimami dhidi ya Muislamu mwingine.”

Iwapo Marekani itaishambulia Saudi Arabia au Imarati, tutasimama pamoja nazo pia

Mwanazuoni huyo wa Misri akisisitiza kwamba; hana uadui wowote na nchi za Ghuba, zikiwemo Saudi Arabia na Falme za Kiarabu (UAE), amesema kwamba msimamo wake umejengwa juu ya misingi ya kidini isiyobadilika, si mielekeo ya kisiasa au tofauti za muda mfupi.

Ameongeza kuwa; iwapo Marekani itaishambulia Saudi Arabia au Falme za Kiarabu, bila shaka atasimama pamoja na nchi hizo, kwa sababu katika fiqhi ya Kiislamu, upande unaovamiwa una haki ya kujilinda kisheria.

Kisha alisisitiza mambo kadhaa muhimu:

1- Kujilinda kisheria: Alitathmini mashambulizi yoyote ya Iran dhidi ya maslahi ya Marekani kuwa yako ndani ya mfumo wa kujilinda kisheria, akisema kwamba haki hiyo inatambuliwa katika fiqhi ya Kiislamu pamoja na sheria za kimataifa.

2- Palestina na Gaza: Aliyakosoa mataifa ya Kiarabu kwa kuwaacha wananchi wa Palestina na Ghaza, na akasema kuwa; Iran angalau inastahili kushukuriwa kutokana na kuunga mkono mhimili wa Muqawama na wananchi wa Palestina.

3- Mabadiliko ya fikra katika nchi za Ghuba: Abdulqawi alikaribisha kuongezeka kwa mitazamo ndani ya Saudi Arabia na Qatar inayopinga kuingia vitani dhidi ya Iran, na akasema mtazamo huo ni ishara ya busara ya kisiasa.

Pia aliwasifu baadhi ya wanafikra wa Kiarabu wanaoamini kuwa mahusiano na Iran hayapaswi kutolewa kafara kwa ajili ya Israel.

Mwishoni mwa mazungumzo yake, mwanazuoni huyo wa Ahlu Sunna wa Misri alisisitiza kwa kusema: “Marekani ni mvamizi dhalimu, na sisi daima tunasimama upande wa anayevamiwa, si upande wa mvamizi, popote ulipo ukweli, nami nitakuwa katika upande huo.” Mwishoni alisisitiza kuwa; tofauti za kimadhehebu na kisiasa hazipaswi kufunika misimamo ya kimaadili na kisheria kuhusu migogoro ya kikanda.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha